Na Lydia Lugakila, Misalaba MediaMgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Tulia Ackson leo tarehe 22 Oktoba, 2025 amefanya ziara kwenye maeneo mbalimbali kwa kuwatembelea wananchi na wafanyabiashara kwa lengo la kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.Dkt. Tulia amewahimiza wananchi hao kushiriki Uchaguzi kwa amani huku akiwasisitiza kukipigia kura za kishindo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia ngazi ya Rais, Wabunge pamoja na Madiwani.








Post a Comment