Baada ya baadhi ya Wananchi kuonesha kuchoshwa na kero ya kusuasua kwa huduma za Mabasi ya Mwendokasi jana usiku na kuamua kushambulia kwa mawe Mabasi na Vituo vinne vya Mabasi hayo, Jeshi la Polisi limesema limewakamata Watu watatu kwa tuhuma za kuharibu miundombinu ya Mabasi ya Mwendokasi.
Taarifa ya Jeshi hilo imenukuliwa ikieleza yafuatayo “Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam tarehe 1 Oktoba 2025 kati ya majira ya saa mbili usiku maeneo ya Gerezani Kariakoo, Magomeni Mapipa, Magomeni Usalama na Magomeni Kagera kwenye Vituo vya Mabasi ya Mwendokasi, baadhi ya Mabasi yalirushiwa mawe na Vituo hivyo baadhi vioo vyake kuvunjwa”
“Watuhumiwa watatu walikamatwa, wanahojiwa na chanzo cha matukio kinafuatiliwa, Watuhumiwa wengine waliohusika katika tukio hilo wanatafutwa, Jeshi la Polisi linawaonya Watu kutojihusisha na matukio ya kihalifu ikiwemo kuharibu miundombinu ya umma” ——— imeeleza taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi Dar es salaam.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment