Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne, amesema mbali na Mabasi ya Mwendokasi na Vituo vinne vya Mabasi hayo kupigwa mawe usiku wa jana, baadhi ya Wananchi hao walifanya fujo katika Vituo viwili vya Polisi ambavyo ni Kituo cha Polisi Magomeni Usalama na Kituo cha Polisi Magomeni Kagera.
Kamanda Muliro amenukuliwa akieleza yafuatayo “Inadaiwa baadhi walifanya fujo kwenye maeneo yale ya Kituo cha Polisi cha Usalama pale na Kagera na kwenye fujo hizo baadhi ya magari yaliharibiwa vioo vyake lakini pia baadhi ya Vituo vile vya eneo lile vilipata madhara ya fujo zile”
“Kwahiyo Polisi walifika na kuweza kudhibiti hali ile pale Maeneo ya Kagera kwasababu Mabasi yalikua yanapandisha kuja Ubungo mpaka kule Kimara, kusema ukweli pamoja na sababu nyingine mbalimbali ambazo zimekuwa zikielezwa lakini swala la kuharibu miundombinu hii ya usafiri ni kosa kisheria kwahiyo hata ukitoa sababu nyingine mbalimbali sisi Wasimamizi wa sheria tunaangalia usalama unaimarika namna gani, kama kuna jamba
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment