" SMAUJATA YAHIMIZA JAMII KUCHANGIA DAMU KUOKOA MAISHA SHINYANGA

SMAUJATA YAHIMIZA JAMII KUCHANGIA DAMU KUOKOA MAISHA SHINYANGA

Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga imeendesha zoezi la kuchangia damu salama kwa lengo la kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga, Nabila Kisendi, amesema kampeni hiyo inalenga kuhamasisha mshikamano wa kijamii kwa kuhakikisha hospitali zinakuwa na hifadhi ya damu ya kutosha kwa ajili ya wahitaji.

Mbali na kuchangia damu, wananchi walioshiriki walipata pia huduma za bure za kupima afya ikiwemo shinikizo la damu (pressure), kiwango cha sukari mwilini pamoja na uchunguzi wa magonjwa mengine ya maisha.

Huduma hizo zilitolewa kwa ushirikiano wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kupitia ofisi ya Mganga Mfawidhi wa Mkoa.

SMAUJATA iliendelea kuwasisitizia wananchi na wadau umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kuchangia damu, kwa kuwa kila tone lina mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya wagonjwa, hususan wajawazito, watoto na wahanga wa ajali.

Zoezi hilo lilifanyika katika eneo la stand ya Hiace, karibu na soko kuu la Mkoa wa Shinyanga.


 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post