"
KINJEKITILE; AHIDI MAJI SAFI, AFYA BORA NA KILIMO CHA KIUCHUMI KUWA VIPAUMBELE VYAKE KILWA KASKAZINI
Na osama Mohamedi chobo ,kilwaMgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kilwa Kaskazini, Mhe. Kinjekitile Ngombale Mwiru, ameahidi kuhakikisha wananchi wa jimbo hilo wanapata huduma bora za kijamii ikiwemo maji safi na salama, huduma bora za afya, pamoja na kuimarisha kilimo cha kisasa chenye tija kwa wakulima.Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Chumo, wilayani Kilwa, Mhe. Kinjekitile alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo, atahakikisha changamoto za upatikanaji wa maji, huduma duni za afya na kilimo cha kizamani zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.Aidha, aliwataka wananchi wa Kilwa Kaskazini kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kumpa kura za kishindo mgombea urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wa ubunge na udiwani, ili kuhakikisha mnyororo wa maendeleo unaendelea bila kukatika.Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Lindi, Patrick Mangarinja, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kilwa, Bi. Hawa Nyoni, pamoja na viongozi wengine wa chama na wananchi
Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kilwa Kaskazini, Mhe. Kinjekitile Ngombale Mwiru.






Post a Comment