" KIOO CHA UAMUZI WA WANANCHI: UTULIVU NA IMANI KATIKA DIRA YA MAENDELEO NDANI YA UCHAGUZI

KIOO CHA UAMUZI WA WANANCHI: UTULIVU NA IMANI KATIKA DIRA YA MAENDELEO NDANI YA UCHAGUZI

Huku Taifa likipiga hatua muhimu ya kidemokrasia kwa kufanya Uchaguzi Mkuu, utafiti wa hivi karibuni wa Kituo cha Sera za Kimataifa Afrika (CIP–Africa) unaonyesha wazi jinsi Watanzania wanavyoendelea kuamini katika mifumo ya kidemokrasia na mwelekeo wa maendeleo wa nchi. Matokeo ya utafiti huu, uliochapishwa hivi karibuni, yanaakisi imani ya umma kwa uwajibikaji na kazi inayoonekana katika sekta mbalimbali.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanyika katika mikoa 19, asilimia kubwa ya Watanzania waliohojiwa—ambayo ni asilimia 83—wamesema watashiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa leo. Idadi hii ni ishara wazi ya ukomavu mkubwa wa kisiasa nchini na uthibitisho kuwa wananchi wanathamini na kuamini katika mchakato wa kura kama njia halali na bora ya kufanya mabadiliko na kuchagua viongozi wanaowataka.

Zaidi ya hayo, utafiti unaripoti kuwa asilimia 91 ya waliohojiwa wameonyesha kuridhishwa na utendaji wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC). Hii inatoa msingi imara kwa maandalizi ya uchaguzi wa kesho, ikionyesha kwamba wananchi wanauona mfumo unaosimamia kura kuwa wa kuaminika.

Utafiti wa CIP–Africa hauakisi tu takwimu, bali unaakisi matokeo ya maendeleo yanayowagusa wananchi moja kwa moja. Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, Serikali imeelekeza rasilimali kubwa katika sekta muhimu za afya,maji na elimu na miundombinu.

Kwenye sekta ya afya,zaidi ya hospitali 250, vituo vya afya 1,200, na zahanati 3,000 zimejengwa kote nchini, hatua iliyoboresha huduma za afya mijini na vijijini.Sekta ya maji imepokea uwekezaji mkubwa, huku uimarishaji wa elimu ukiendelea kupitia mpango wa elimu bila malipo na ujenzi wa shule mpya 1,500. Kwenye miundombinu kumekuwa na upanuzi wa barabara kuu, madaraja, na reli ya kisasa (SGR) kazi iliyowezesha kuanza kwa fursa za ajira na uwekezaji, na kuunganisha mikoa yote ya nchi.

Maendeleo haya yametajwa kama sababu kuu inayojenga imani kubwa kwa wananchi. Kura ya maoni hii haikuja kama muujiza; imebeba hisia za watu walioguswa na maboresho ya huduma za kijamii, ikionyesha ukweli wa kazi inayoonekana na uwajibikaji.

Kutokana na utafiti huo ambao unatumika kama dira ya Uchaguzi Mkuu wa kesho Watanzania wameeleza wazi wanachokitaka—maendeleo, utulivu na uongozi unaojali. 

Post a Comment

Previous Post Next Post