Na Mwandishi wetu
Tanzania inaendelea kupiga hatua kubwa katika kuinua uchumi wake, huku miradi mikubwa ya kimkakati, hasa ile inayohusu miundombinu, ikionekana kuchochea fursa mpya za biashara na uwekezaji.
Wakati nchi ikielekea katika kipindi cha uchaguzi, serikali imeweka bayana kuwa maamuzi ya kusaka uwekezaji wa kimataifa yameanza kuzaa matunda yanayoonekana wazi.
Serikali kupitia msemaji wake Gerson Msigwa amekuwa akieleza mafanikio na hivyo Watanzania wanapaswa kutuliza vichwa kuelewa kinachoendelea na kutambua kuwa mikataba yote imefanyika kwa mujibu wa sheria za nchi na kwa nia ya kuleta manufaa ya muda mrefu kwa taifa.
Maamuzi haya ni sehemu ya mkakati mpana wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati na yenye ushindani wa kiuchumi duniani. Katika kipindi hiki cha uchaguzi, ni muhimu kwa wananchi kufanya maamuzi yenye tija kwa kuangalia mafanikio ya kiuchumi yanayoletwa na uwekezaji wa kimkakati, kwani kura ni mwanga wa maendeleo.Jumla ya maamuzi haya ya uwekezaji yanachochea ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) na kuimarisha mazingira ya biashara nchini.
Kauli hizi za mafanikio zimeungwa mkono na wasomi na wataalamu wa uchumi. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waisilamu Morogoro (MUM), Profesa Mussa Assad, amesema miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imewezesha uchumi kukuwa hadi asilimia sita, huku mfumuko wa bei ukiwa mzuri.
Profesa Assad alitoa kauli hiyo wakati wa Kongamano la Kitaaluma Kujadili Utekelezaji wa Uchumi Jumuishi kufikia 2050 lililoandaliwa na MUM kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC).
Alisema kutokana na kuimarika kwa uchumi, uwezo wa kiuchumi nao umeimarika.
Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila, aliongeza kuwa uongozi wa Rais Samia umechangia ajira nyingi kuongezeka kwenye sekta mbalimbali.
Miradi Mikubwa ya Miundombinu Inavyoinua Tija
Kupitia programu ya DMGP, Serikali imeboresha gati namba 1–7 kwa kuongeza kina kutoka mita 8 hadi 14.5, sambamba na kuimarisha eneo la kugeuzia meli kwa kina cha mita 15, huku lango la kuingilia likipanuliwa.
Aidha Uamuzi wa serikali kuingia makubaliano ya usimamizi wa baadhi ya gati katika Bandari ya Dar es Salaam na Kampuni ya DP World ya Dubai, umeleta mageuzi makubwa katika sekta ya uchukuziUwekezaji huu uliolenga kupunguza muda wa meli kusubiri bandarini (turnaround time) na kuongeza kasi ya upakuaji na upakiaji wa mizigo umewezesha .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo, akiwasilisha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/26 alieleza mafanikio kumi yaliyopatikana baada ya Kampuni ya DP World kuendesha sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam.
Ongezeko hili la tija linawezesha bidhaa za Tanzania na za nchi jirani kufika sokoni kwa haraka na kwa gharama nafuu. Kuboresha bandari kunaimarisha hadhi ya Dar es Salaam kama kitovu kikuu cha biashara (Regional Hub) kwa nchi jirani zisizo na bandari, jambo linalomaanisha ongezeko la mapato ya forodha na tozo za huduma kwa serikali. Mifumo thabiti ya udhibiti na usalama inayohusisha Mamlaka ya Bandari (TPA) na Mamlaka ya Mapato (TRA) ipo kwa ajili ya kuhakikisha rasilimali zote zinazopitia bandarini zinakaguliwa na kutoa mapato stahiki ya kodi.
Vilevile, hatua ya kuelekea katika ubia wa usimamizi au uwekezaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), imelenga kupanua wigo wa huduma na abiria. Uboreshaji wa KIA utahamasisha ndege kubwa zaidi za kimataifa kutua moja kwa moja Kaskazini mwa Tanzania. Hili litaongeza idadi ya watalii wanaotembelea Hifadhi za Taifa na Mlima Kilimanjaro, na hivyo kuongeza mapato ya fedha za kigeni kutokana na sekta ya utalii.
KIA ni lango muhimu pia kwa usafirishaji wa madini ya thamani kama vile Tanzanite. Kuimarika kwa usimamizi na usalama kutahakikisha kuwa rasilimali hizi zinasafirishwa kupitia njia rasmi, huku ukaguzi mkali wa Mamlaka ya Madini (TMAA) na vyombo vya usalama ukisimamia biashara hiyo ili kuzuia utoroshaji.
Post a Comment