Na Mwandishi Wetu.
Mwanaharakati wa mitandaoni, Mange Kimambi, amejikuta katika hali ya aibu baada ya maandamano aliyoyatisha nchini Marekani tarehe 17 Oktoba 2025 kushindwa kuvutia umati kama alivyotarajia.
Licha ya kufanya kampeni kubwa kupitia mitandao ya kijamii na kutoa ahadi kwamba Watanzania wengi wanaoishi Marekani wangekwenda kumuunga mkono, tukio hilo lilishuhudia mahudhurio duni, hali iliyoashiria ukosefu wa uungwaji mkono wa kweli.
Tukio hilo limebainisha ukweli kwamba sauti kubwa mtandaoni si kigezo cha ushawishi katika uhalisia. Mange, ambaye amejitambulisha kwa muda mrefu kama msemaji wa wananchi, inaonekana hakusoma kwa usahihi mtazamo na hisia za Watanzania wanaoishi nje ya Nchi kuhusu ajenda zake za kisiasa na kijamii.
Wengi wa Watanzania wanaoishi Marekani wameonekana kuchoshwa na siasa za majukwaa ya mtandao na badala yake wanaunga mkono mabadiliko ya kweli yanayoendelea kufanywa nchini Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa ujumla, kushindikana kwa maandamano hayo ni somo muhimu kwa wanaharakati wote kwamba nguvu ya maneno mtandaoni haiwezi kuchukua nafasi ya vitendo halisi.
Ni wazi kwamba watanzania wanatakiwa kutafakari kwa kina kile kilichotokea Marekani na uhalisia wa mambo kwani wao ndiyo hasa wanaoshuhudia maendeleo yanayoendelea kuonekana kuliko hao walioko nje ya Nchi.
Post a Comment