" MR. BLACK AREJESHA MATUMAINI KATIKA ELIMU SHINYANGA, ATOA MSAADA WA VIFAA KWA SHULE 9 ZA MSINGI

MR. BLACK AREJESHA MATUMAINI KATIKA ELIMU SHINYANGA, ATOA MSAADA WA VIFAA KWA SHULE 9 ZA MSINGI

Na Elisha Petro, Misalaba Media

Mkurugenzi wa The BSL Investments Company Limited na mmiliki wa BSL Schools Tanzania na Rwanda, Ndugu Peter A. Frank Lugumi (maarufu kama Mr. Black), leo Oktoba 3, 2025 amerejesha tabasamu kwa walimu na wanafunzi wa shule za msingi mkoani Shinyanga baada ya kutoa msaada wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3.8.

Mr. Black, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya darasa la saba shule ya msingi Ibinzamata, ametumia fursa hiyo kutekeleza wajibu wake wa kijamii (CSR) kwa kusaidia shule tisa za msingi za mkoa huo.

Msaada alioutoa unajumuisha:

  • Tani moja na nusu ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa madarasa, ujenzi wa ukuta na vyoo katika shule za msingi Kambarage, Nhelegani na Town.

  • Seti za jezi kamili kwa shule za msingi Bugayambelele, Kizumbi na Ibinzamata.

  • Mipira minne ya soka kwa ajili ya michezo katika shule nne tofauti.

  • Viti 15 vya walimu kwa shule za msingi Kitangiri, Ibinzamata, Ushirika na Mapinduzi B.

  • Tripu mbili za mchanga kwa shule ya msingi Kizumbi.

  • Ndoo za rangi kwa shule za msingi Bugoyi na Mapinduzi B.

  • Ngano kwa ajili ya chai ya walimu wa shule ya msingi Ibinzamata.

Thamani ya msaada huo ni shilingi 3,857,000.

Mr. Black amesema mchango huo ni ishara ya kuunga mkono juhudi za serikali na jamii katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Ameongeza kuwa elimu ni nyenzo muhimu ya maendeleo hivyo kila mdau anapaswa kushiriki katika kuiboresha.

Aidha, ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kusapoti sekta ya elimu mkoani Shinyanga kwa manufaa ya watoto na vizazi vijavyo.






 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post