Na Osama Chobo, Misalaba Media -Songea Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linawashikilia watu 15 kwa tuhuma za mauaji ya watu watano na kujeruhi wengine watatu katika tukio la kujichukulia sheria mkononi lililotokea Oktoba 1, 2025, majira ya saa saba usiku katika kitongoji cha Likologo, kijiji cha Wenje, kata ya Nalasi Magharibi, Wilaya ya Tunduru. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Chilya, amesema kuwa majina ya watuhumiwa yamehifadhiwa kwa sababu za kipelelezi huku upelelezi ukiendelea ili kuwakamata wote waliohusika.Tukio hilo limetokana na mgogoro kati ya wakulima na wafugaji ambapo chanzo chake kilianzia Septemba 30, 2025, saa 11 jioni, baada ya mkulima aitwaye Hassan Mponda Moshi kushambuliwa na mfugaji ambaye bado hajafahamika. Tukio hilo limesababisha hasira kwa wananchi wa vijiji vya Nakapunda na Wenje ambapo usiku wa Oktoba 1, takribani wananchi 100 walienda kwenye makazi ya wafugaji na kuwakuta wamekimbia, kisha kufungua ng’ombe zizini, kuwaua, kuwachuna ngozi na kuchukua nyama.Katika hali isiyotarajiwa, wananchi hao walipokuwa wakirejea majumbani mwao na mizigo ya nyama, walivamiwa na kundi la wafugaji waliokuwa na silaha za jadi kama mapanga na mikuki na kuanza kuwashambulia. Shambulio hilo limepelekea vifo vya watu watano waliotambulika kuwa ni Mfaume Machaka Ally (68), Imani Saidi Abdu Kosa (50), Abdalah Ally Biashara (37), Mipango Mihoba Mwituta (54), na Hamisi Husein Shaibu (13), huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya.Majeruhi wa tukio hilo ni Jana Saidi Athuman (48), Alifa Salumu Mbahu (49), na Mahala Rajabu Mahala (56), ambao kwa sasa wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mission Mbesa. Miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi wa kidaktari na kukabidhiwa kwa familia kwa taratibu za mazishi.Kamanda Chilya ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kufuata taratibu za kisheria kwa kushirikisha viongozi wa serikali za mitaa, vijiji pamoja na jeshi la polisi ili kutatua migogoro kwa njia ya amani. Aidha, amehimiza ushirikiano wa raia wema na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa mapema ili kuzuia uhalifu na kudumisha amani katika jamii.

Post a Comment