" TAHADHARI KWA WANANCHI: DUMISHA AMANI NA KUFUATA SHERIA

TAHADHARI KWA WANANCHI: DUMISHA AMANI NA KUFUATA SHERIA

Wananchi wote wa Tanzania wanatakiwa kutahadharishwa kuhusu vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga amani na utulivu wa nchi, hasa vile vinavyochochewa na maslahi binafsi au watu walio nje ya mfumo wa kisheria wa nchi.

Maneno yoyote au wito unaohamasisha wananchi kukiuka sheria, kuvuruga utaratibu wa uchaguzi, au kufanya vitendo vya ghasia ni kinyume cha sheria.

Epuka uchochezi unaolenga kuvuruga utaratibu uliopo, kwani vitendo hivyo vinaweza kuhatarisha maisha yako na ya wenzako na kupelekea kuchukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yako.

Tunawahimiza Watanzania wote kutumia hekima, kudumisha utulivu, na kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kujitokeza kwa amani kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025 na kurudi majumbani mwao kusubiri matokeo kwa utulivu na kwa mujibu wa sheria.

Mabadiliko ya kweli hupatikana kwenye sanduku la kura, si kwenye ghasia.

Amani na utulivu ni msingi mkuu wa taifa letu. Maendeleo yoyote ya kweli yanajengwa juu ya amani, kwani machafuko, ghasia, na uharibifu huleta hasara kubwa kwa uchumi, jamii, na huchelewesha maendeleo kwa vizazi vijavyo. Amani ya kweli hupatikana kwa kufuata sheria, si kwa vurugu.

Njia pekee, salama, na ya kisheria ya kufanya mabadiliko ya uongozi, katiba, au sheria ni kupitia mfumo wa kikatiba uliowekwa. 

Kupiga Kura: Hii ndiyo silaha kuu na ya kisheria ya kuleta mabadiliko ya uongozi, kama alivyohimiza Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Kutumia Bunge: Hiki ni chombo halali cha kutunga sheria na kufanya mabadiliko ya Katiba kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Mahakama: Kutatua migogoro yote ya kisheria na uchaguzi kunapaswa kufanyika kupitia Mahakama.

Wito Mkuu: Kataa Uchochezi, Linda Maisha Yako

Post a Comment

Previous Post Next Post