" TAKUKURU YAWAPA MAFUNZO WAANDISHI WA HABARI KAGERA KUHUSU MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA WAKATI WA UCHAGUZI

TAKUKURU YAWAPA MAFUNZO WAANDISHI WA HABARI KAGERA KUHUSU MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA WAKATI WA UCHAGUZI


Na Lydia Lugakila – Misalaba Media, Kagera

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imeendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa habari kuhusu mapambano dhidi ya rushwa wakati wa uchaguzi, huku ikiwakumbusha umuhimu wa kuzingatia miiko na maadili ya taaluma yao.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, Vangsada Mkalimoto, amesema lengo kuu ni kuwaongezea waandishi uelewa juu ya wajibu wao katika kuzuia na kupambana na rushwa, sambamba na kuelimisha jamii kuhusu madhara yanayotokana na vitendo hivyo.

"Waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika jamii nawashauri mzingatie miiko ya kazi zenu za habari, na mtumie kalamu zenu kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, wa amani na wa haki,” alisema Mkalimoto.

Mada zilizojadiliwa katika mafunzo hayo zilihusisha

wajibu wa waandishi wa habari katika mapambano dhidi ya rushwa wakati wa uchaguzi

Makosa ya rushwa katika Sheria ya Uchaguzi ya Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024, makosa ya rushwa katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi Na. 6 ya mwaka 2010.

Kupitia mafunzo hayo, TAKUKURU imesisitiza dhamira yake ya kushirikiana na vyombo vya habari kuhakikisha jamii inapata elimu sahihi kuhusu rushwa, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu

 

Post a Comment

Previous Post Next Post