"
WANANCHI KATA YA TINGI WAHAMASISHANA KUPIGA KURA KUPITIA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU
Wananchi wa Kata ya Tingi, wilayani Kilwa, wamejitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la uchangiaji damu lililofanyika leo katika Kituo cha Afya cha Tingi, ikiwa ni sehemu ya hamasa kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika kesho, Oktoba 29.Zoezi hilo limehusisha wananchi pamoja na viongozi wa kisiasa, likilenga kuonesha mshikamano na upendo wa kijamii, sambamba na kuhamasisha ushiriki katika zoezi la upigaji kura.Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, mratibu wa zoezi hilo ambaye pia ni mgombea wa Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema kuwa uchangiaji damu ni sehemu ya huduma kwa jamii na unalenga kuwasaidia wale wenye uhitaji.Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, Mheshimiwa Kinjkitile Ngombale Mwiru, aliwataka wananchi wote waende kwa amani kesho kushiriki katika upigaji kura. “Zoezi hili la uchangiaji damu limeonesha umoja na uzalendo. Naomba wananchi waendelee na moyo huu wa kujitokeza kwa wingi kesho katika zoezi la kupiga kura,” alisema Mwiru.Akizungumza kwa niaba ya wananchi walioshiriki, Manzi Abdallah, alisema kuwa wamefanya tukio hilo si tu kwa lengo la kusaidia wagonjwa, bali pia kuhamasishana kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi.Zoezi hilo la uchangiaji damu limefanyika chini ya kauli mbiu maalum isemayo: “Changia Damu okoa maisha shiriki uchaguzi oktoba 29 Tunza amani ni tunu ya nchi yetu "
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, Mheshimiwa Kinjkitile Ngombale Mwiru, akichangia damu salama.







Post a Comment