Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga kimetoa pongezi kwa Mhe. Salome S. Makamba kufuatia uteuzi wake kuwa Naibu Waziri wa Nishati, uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Viongozi wa chama hicho wamesema uteuzi huo ni ishara ya imani kubwa aliyopewa kutokana na uwezo na utendaji wake katika nafasi mbalimbali alizowahi kushika. Wakisema wanaamini kuwa Wizara ya Nishati itanufaika na weledi wake.
Aidha, CCM Shinyanga imeahidi kuendelea kumuunga mkono katika majukumu yake mapya, wakiongeza kuwa wanaamini ataongeza kasi ya miradi ya nishati na kuimarisha huduma za umeme katika maeneo mbalimbali nchini.

Post a Comment