
Na Lydia Lugakila, Misalaba MediaMbeyaTaasisi ya Tulia Trust iliyopo chini ya Mbunge wa Jimbo la Uyole jijini Mbeya, Dkt. Tulia Ackson, imeanza ujenzi wa nyumba ya familia ya mzee Anyomwisye Mwalyaje, mkazi wa mtaa wa Mwafute, kata ya Ilemi,Mkoani Mbeya ambayo iliteketea kwa moto usiku wa Septemba 5,2025 kutokana na hitilafu ya umeme.Hatua hiyo imekuja baada ya Dkt. Tulia kutoa ahadi ya kumjengea upya mzee Mwalyaje alipomtembelea mara tu baada ya tukio hilo ambalo liliharibu kabisa nyumba pamoja na mali zote zilizokuwemo ndani.Afisa Habari wa Taasisi ya Tulia Trust, Addi Kalinjila, amesema ujenzi huo umeanza mara moja baada ya vifaa kufikishwa katika eneo la ujenzi, ikiwa ni jitihada za kurejesha maisha ya familia hiyo na kuhakikisha wanapata makazi salama kama ilivyokuwa awali.Nao baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mwafute wameipongeza hatua hiyo wakisema kuwa inaonesha namna ambavyo uongozi wa Dkt. Tulia umeendelea kugusa maisha ya watu wanaopitia changamoto mbalimbali. Aidha Wamesema msaada huo utairejeshea familia hiyo matumaini ambayo yalipotea baada ya kupoteza makazi yao.Kwa upande mwingine, viongozi wa eneo hilo wametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya hitilafu za umeme kwa kuhakikisha mifumo ya nyumbani inafanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara.Hata hivyo wameongeza kuwa ushirikiano kati ya jamii na taasisi kama Tulia Trust ni muhimu katika kukabiliana na majanga na kusaidia wananchi wanaoathirika.


















Post a Comment