
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga imetangaza kuanza kwa zoezi la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) bure katika Uwanja wa Nguzonane (FIRE) kuanzia Novemba 11 hadi 15, 2025.
Zoezi hilo litafanyika kila siku kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni, likilenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kujitambua kiafya na kuchukua hatua mapema katika kudhibiti magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu na uzito kupita kiasi.
Wakati wa zoezi hilo, wananchi watapatiwa huduma za uchunguzi pamoja na ushauri wa kitaalam kuhusu lishe na mtindo bora wa maisha bila malipo. Hospitali hiyo imewahimiza wakazi wa Manispaa ya Shinyanga na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hizo.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment