"
MAHAFALI YA 23 CHUO CHA BIBLIA MBEYA YAFANA WAHITIMU WAASWA KUSIMAMA IMARA DHIDI YA MAFUNDISHO POTOFU
Na Lydia Lugakila, Misalaba Media -MbeyaWahitimu wa mafunzo ya Biblia kutoka Chuo cha Kanisa la Pentecostal Holiness Mission mkoani Mbeya wamesisitizwa kujiepusha na mafundisho potofu yanayoweza kuwafanya kutotekeleza kazi ya Mungu kwa usahihi.Akizungumza katika mahafali ya 23 ya chuo hicho yaliyofanyika Novemba 19,2025 mkuu wa Chuo, Mchungaji Timothy Ibrahim, amesema mafundisho yasiyo sahihi yamekuwa mengi katika jamii, hivyo ni wajibu wa wahitimu kuyatambua na kuyaepuka ili waweze kuvuna matunda mema yatakayowaongoza kufikia ufalme wa Mungu.Aidha, Mchungaji Ibrahim amewasisitiza wahitimu kufanya kazi ya Mungu kwa uaminifu na moyo mkunjufu, akieleza kuwa uaminifu huo ndio utakaowaletea baraka tele katika maisha yao.Akiwasilisha taarifa ya chuo, amesema kuwa kwa sasa kina jumla ya wanafunzi 51: mwaka wa kwanza 10, mwaka wa pili 29, na mwaka wa tatu 12 ambapo chuo kilianzishwa mwaka 1996, na kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vitanda, viti, kutokukamilika kwa baadhi ya vyumba, pamoja na uhaba wa fedha kutokana na vyanzo duni vya mapato, hali inayowalazimu baadhi ya watumishi kujitolea.Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Elimu na Vyuo Taifa, Fabian Sanga, amesema moja ya majukumu ya idara hiyo ni kuhakikisha mazingira ya kujifunzia na kufundishia yanaboreshwa ili wanafunzi wapate elimu katika mazingira mazuri.Alisisitiza umuhimu wa wahitimu kujiendeleza kielimu kwa kuwa dunia inabadilika kila siku “lakini Biblia haibadiliki,” alisema."Dunia ya sasa si salama; inahitaji mimi na wewe tukahubili injili ili kurejesha ile salama inayotakiwa sasa hadi mwisho wa dunia," alisema Sanga.Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Holiness Mission, Mchungaji Festo Ntobanga Mwasyove, amewataka wahitimu kuhakikisha majina yao yanaandikwa mbinguni, akisema matendo mema ndio yatakayowafikisha huko.Askofu Mkuu ametoa mfano wa safari yake ya huduma na jinsi alivyoweka bidii katika ujenzi wa makanisa mengi, akiwataka wahitimu kujiandaa kutumika kwa bidii na utii.Katika Risala iliyosomwa na wahitimu akiwemo Asajile Mwakalasya, walibainisha changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na uhaba wa magodoro, vitanda, kompyuta moja, na kutokukamilika kwa ofisi tatu muhimu za chuo.Walisema chuo hicho kimezalisha watumishi wengi wanaohudumu maeneo mbalimbali nchini, na kwa mwaka huu wa 2025 wanafunzi wa stashahada ni 12, na wa shahada ni 29, jumla 41 kati ya 51, huku wakitamani kuona chuo kinapanda daraja hadi kutoa elimu ya juu zaidi kwa jamii.Naye mgeni rasmi Mchungaji Lawi Julias, alijibu baadhi ya changamoto hizo kwa kuchangia kiasi cha fedha na kuongoza harambee, akitoa wito kwa jamii na kanisa kuendelea kujitolea ili kuisukuma mbele kazi ya Mungu.
























Post a Comment