" MKURUGENZI WA MALULA TV ASHUKURU MWALIKO WA KUHUDHURIA UAPISHO WA MBUNGE KATAMBI JIJINI DODOMA

MKURUGENZI WA MALULA TV ASHUKURU MWALIKO WA KUHUDHURIA UAPISHO WA MBUNGE KATAMBI JIJINI DODOMA

 


Na Marco Maduhu.
×××××
MKURUGENZI wa kituo cha televisheni cha mtandaoni Malula TV Online kilichopo mkoani Shinyanga, Daniesa Malula, amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, kwa kumualika kushuhudia tukio la kuapishwa kwake bungeni jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya hafla hiyo, Malula amesema amefarijika kwa heshima hiyo aliyopewa na mbunge huyo, akibainisha kuwa ni ishara ya ushirikiano mzuri kati ya viongozi na wadau wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga.

“Ninamshukuru sana Mhe. Katambi kwa kunikaribisha kushuhudia tukio hili muhimu, ni heshima kubwa kwangu na kwa Malula TV kwa kutambuliwa kama sehemu ya wadau wa maendeleo katika jimbo la Shinyanga,” amesema Malula.

Aidha, ametumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Katambi kwa kuapishwa rasmi kuwa mbunge wa Shinyanga Mjini, akimtakia utekelezaji mwema wa majukumu yake ya kuwawakilisha wananchi bungeni.

“Ninampongeza Mhe. Katambi kwa kuapishwa kwake. Tunamwamini kama kiongozi kijana mwenye dira na uchapakazi, na tupo tayari kushirikiana naye katika kutoa taarifa na kuelimisha jamii kupitia vyombo vya habari,” aliongeza.

Mhe. Katambi aliapishwa bungeni jijini Dodoma baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29,2025

Post a Comment

Previous Post Next Post