Na Mapuli Kitina Misalaba
Zoezi la Samia Ardhi Kliniki limeendelea katika
viwanja vya Soko Kuu la Mkoa wa Shinyanga, ambapo huduma mbalimbali za masuala
ya ardhi zinatolewa, ikiwemo utoaji wa hati miliki papo kwa papo.
Akizungumza katika eneo la zoezi hilo, Mthamini kutoka
Ofisi ya Kamishna Msaidizi Mkoa wa Shinyanga, Neema Augustine Mbaga, amesema
kliniki hiyo ilianza Machi 2 na itahitimishwa Machi 7, 2026, ikitoa fursa kwa
wananchi hususan wanawake kupata huduma za umiliki wa ardhi kwa urahisi.
“Tupo hapa katika viwanja vya Soko Kuu
tangu tarehe 2 na tutaendelea hadi tarehe 7. Tunatoa huduma mbalimbali ikiwemo
utoaji wa hati miliki papo kwa papo. Wananchi wote wanahudumiwa lakini akina
mama wamepewa kipaumbele maalum,” amesema Mbaga.
Ameeleza kuwa huduma zinazotolewa ni pamoja na ushauri
wa masuala ya ardhi, utatuzi wa migogoro kupitia mabaraza ya ardhi ya wilaya,
uthamini wa mali, upimaji na ramani, pamoja na ushauri kuhusu vibali vya ujenzi
na mipango miji na kwamba Masaveya pia wanatembelea maeneo yenye changamoto za
mipaka kwa ajili ya marekebisho.
Kwa upande wake, Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa
Shinyanga, Emmanuel Gwaltu, amesema tayari baadhi ya wanawake wameandaliwa na
kukabidhiwa hati miliki zao huku elimu ya masuala ya ardhi ikiendelea kutolewa
kwa wote wanaofika katika kliniki hiyo.
“Wapo wanawake ambao waliomba kumilikishwa ardhi
zao, tayari tumewaandalia hati na baadhi yao tumewakabidhi. Tunaendelea kutoa
elimu ili kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kumiliki ardhi kisheria,”
amesema Gwaltu.
Afisa Ardhi Mwandamizi Mkoa wa Shinyanga, Halima
Mrinji, amesema lengo la zoezi hilo ni kuwainua wanawake kiuchumi kupitia
umiliki halali wa ardhi.
Naye Afisa Ardhi Mwandamizi wa Manispaa ya Shinyanga,
Lela Amos Chipanyaga, amesema mwitikio ni mkubwa ambapo zaidi ya wanawake 30
walihudumiwa siku ya kwanza na zaidi ya 40 siku ya pili, baadhi wakikabidhiwa
hati zao na wengine kuandaliwa malipo ya gharama za umilikishaji.
Baadhi ya wanufaika wa zoezi hilo ni Judiya Kabendela
wa Majengo Mapya, Wingwe Yohana mkazi wa Shinyanga na Alistiles Njunwa wa Kata
ya Lubaga, ambao wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kumiliki ardhi zao
kisheria.
Zoezi hilo linafanyika kuelekea kilele cha maadhimisho
ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 8, 2026, chini ya kauli mbiu
isemayo: “Mwanamke haki yao milki Ardhi yako sasa.” Mkoa wa Shinyanga
utaadhimisha siku hiyo kimkoa katika Halmashauri ya Ushetu.
Wananchi wakipata huduma mbalimbali za ardhi katika Samia Ardhi Kliniki inayoendelea Viwanja vya Soko Kuu Shinyanga.
Maafisa ardhi wakitoa ushauri, upimaji na huduma za uthamini kwa wananchi waliojitokeza katika Samia Ardhi Kliniki.

Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Gwaltu, akikabidhi hati miliki kwa mmoja wa wanufaika wa Samia Ardhi Kliniki Shinyanga.
Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Gwaltu, akikabidhi hati miliki kwa wanufaika wa Samia Ardhi Kliniki Shinyanga.
Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Gwaltu, akikabidhi hati miliki kwa mmoja wa wanufaika wa Samia Ardhi Kliniki Shinyanga.
Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Gwaltu, akikabidhi hati miliki kwa mmoja wa wanufaika wa Samia Ardhi Kliniki Shinyanga.
Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Gwaltu, akikabidhi hati miliki kwa mmoja wa wanufaika wa Samia Ardhi Kliniki Shinyanga.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment