Serikali ya wilaya ya nyasa mkoani Ruvuma imekabidhi mabati 124, migongo na misumari kwa wananchi waliopoteza makazi yao kufuatia mvua zilizoambatana na upepo mkali zilizonyesha Januari 6, 2026. Msaada huo unalenga kuwasaidia waathirika kurejesha makazi yao baada ya nyumba zao kuharibiwa vibaya na maafa hayo.
Mvua hizo zilisababisha jumla ya nyumba 30 kuathirika katika Kata ya Tingi, zilizojumuisha nyumba 22 katika Kijiji cha Lulimbo na nyumba 8 katika Kijiji cha Tingi. Wananchi wengi walibaki bila makazi salama baada ya paa za nyumba zao kung’olewa na upepo mkali, hali iliyosababisha uhitaji wa haraka wa msaada wa vifaa vya ujenzi.
Akikabidhi msaada leo Februari 3, 2026 katika Ofisi ya Kata ya Tingi, DC Magiri amewashukuru wadau mbalimbali kwa kujitokeza na kuchangia vifaa hivyo muhimu. Amesema ushirikiano kati ya serikali na wadau umeonesha mshikamano mkubwa katika kipindi cha changamoto, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kusaidiana wakati wa majanga.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Khalid Khalif, amesema tayari maelekezo yametolewa kwa viongozi wa kata ili kuhakikisha msaada huo unagawiwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya waathirika. Ameongeza kuwa Kamati ya Maafa ya Wilaya inaendelea kukusanya michango na kutafuta rasilimali zaidi ili kuhakikisha wananchi wote walioathirika wanapata msaada unaostahili.
Kwa upande wao wananchi waliopata maafa hayo meishukuru serikali ya wilaya kwa kuweza kuwaona na kuahidi kufata taratibu za kitaalum waliopewa ili kuweza kuwa salama muda wote
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment