Na, Egidia Vedasto,
Misalaba Media, Arusha.
TANESCO mkoani Arusha wameahidi kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wake, ikiwemo kubadilisha nguzo, kufunga mita za kisasa na kuendelea kutoa elimu kila wakati kwa wateja wake kupitia vyombo mbalimbali vya habari, mbao za ofisini na mitandao ya kijamii.
Akizungumza na Chombo hiki ofisini kwake Jijini Arusha Afisa uhusiano na huduma kwa wateja TANESCO Fredy Mbavai amesema kwa sasa wanajivunia wananchi wanapata huduma safi na malalamiko ya kukatika kwa umeme yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Amesema "Tutaendelea kuboresha huduma zetu kila wakati lengo ni wananchi wapate huduma stahiki, wafanye shughuli zao kwa wakati na kukuza uchumi wao".
Pia amewakumbusha wateja kuwa na matumizi sahihi ya umeme kama vile kuepuka kufunga vifaa ambavyo sio imara, kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mfumo wa waya ndani ya nyumba na kutoa taarifa za wizi wa umeme kila inapobainika.
Mmoja wa wateja mwenye makazi yake Kata ya Olasiti Jijini Arusha Daud Msuya amekiri kuwepo kwa mabadilko makubwa katika upatikanaji wa huduma ya umeme.
Amesema"Mimi kazi yangu ni Kinyozi, siku za nyuma hali ilikuwa mbaya kwa sababu kazi yangu inategemea umeme, umeme ulikuwa ukikatika siku nzima bila majibu lakini kwa sasa tunashukuru maboresho ni makubwa na yanaonekana"
Vilevile Rehema Juma anayefanya kazi Internet Cafe mjini kati ameeleza"Siku za nyuma ilikuwa umeme unakatika bila taarifa na ukipiga simu hupewi majibu ya kueleweka, kwa sasa ukija mjini unafanya kazi na pesa inaonekana, hata kukitokea hitilafu tunapewa taarifa kwa wakati, nawashukuru sana TANESCO kwa kazi kubwa" .
Hata hivyo ameomba huduma ya mita za kisasa kuharakishwa ili kuondoa mkanganyiko hususan kwa wafanyabiashara na wanaoishi nyumba za kupanga
Mwisho.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment