Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Mhe. Salome Makamba kuwa Mbunge wa Viti Maalum, nafasi inayotokana
na uteuzi wa chama hicho tawala kupitia orodha ya wanawake.
Uteuzi huo umefanyika
Novemba 7, 2025 ambapo Wananchi pamoja na wanachama wa CCM wameendelea
kumpongeza kwa uteuzi huo, wakieleza kuwa ni mwanamke mwenye bidii, uadilifu na
mchango mkubwa katika kuimarisha chama na kuwatumikia wananchi.
Kupitia mitandao ya kijamii, salamu nyingi za pongezi
zimekuwa zikimiminika zikionesha matumaini kwamba ataendeleza juhudi za
kuwakilisha kwa ufanisi sauti za wanawake bungeni.
Post a Comment