" STADE MALIEN YAWAZIMA SIMBS SC CAF

STADE MALIEN YAWAZIMA SIMBS SC CAF








Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamelazimika kukubali kichapo cha mabao 2–1 dhidi ya Stade Malien katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2025/26.

Wenyeji walipata bao la kuongoza dakika ya 16 kupitia Taddeo Nkeng, kabla ya kuongeza la pili dakika ya 23 lililofungwa na Ismail Simpara, na kuwapa pointi tatu muhimu katika uwanja wao wa nyumbani.

Simba SC ilipata bao pekee dakika ya 53 kupitia kwa Neo Maema, lakini juhudi za kusawazisha hazikuzaa matunda licha ya kutengeneza nafasi kadhaa za wazi.

Huu unakuwa ni mchezo wa pili mfululizo kwa Simba SC kupoteza kwenye michuano ya kimataifa, ikikabiliwa na changamoto ya kutotumia fursa ilizopata, kwani katika mechi hizi mbili imefanikiwa kupata bao moja pekee dhidi ya nafasi zaidi ya tatu ilizotengeneza.

Katika dakika za mwishoni, mambo yaliendelea kuwa magumu kwa Wekundu wa Msimbazi baada ya kiungo wao Kanté kuonyeshwa kadi nyekundu, hivyo timu ikalazimika kumaliza mchezo ikiwa pungufu

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post