" TARURA NYAMAGANA KUTUMIA ZAIDI YA BILION 6 MATENGENEZO MIUNDOMBINU

TARURA NYAMAGANA KUTUMIA ZAIDI YA BILION 6 MATENGENEZO MIUNDOMBINU


Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaWakala wa barabara vijijni na mjini (TARURA) wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza imeidhinishiwa bilioni 6.5 kwa mwaka 2025/26 kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu yake katika eneo hilo.Meneja wa TARURA wilayani Nyamagana Mhandisi Dunstan Kishaka alisema hayo Leo jijini Mwanza kuwa kwa kuanza tayari serikali kupitia mfuko wa barabara imeidhinisha bilioni 1.7 kutekeleza miradi mitano katika eneo hilo.Alisema miongoni mwa shughuli zitakazofanywa ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika maeneo tofauti jijini hapa pamoja, kutengeneza mitaro kuzuia maji kutuwama juu ya barabara na kuweka taa za barabarani.Mhandisi Kishaka aliongeza kusema kuwa barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ni katika mtaa wa Shadi yenye urefu wa mita 200, barabara ya Buhongwa Bulale urefu wa mita 200 kwa milioni 385.Aliongeza kusema kuwa barabara zingine zitakazojengwa ni Isamilo kuelekea kwa Mkuu wa wilaya yenye urefu wa mita 200, Mwananchi kwenda Mahina urefu wa mita 300 na Bismark mita 200.Mhandisi Kishaka alisema kuna changamoto ya watu kutupa taka kwenye mitaro na hivyo kusababisha kuzibika kwa mitaro hivyo kushindwa kupitisha maji na kusababisha barabara kujaa maji vipindi vya mvua.Aliongeza kusema kuwa changamoto nyingine ni kuwepo kwa malalamiko yanayotolewa na wananchi nyakati za ujenzi na urekebishaji wa mitaro kwani kila eneo likiguswa kwa ajili ya marekebisho huibuka malalamiko ya kuingiliwa katika maeneo yao.Mhandisi Kishaka aliwataka wananchi kujiepusha na uharibifu wa miundombinu kwa kuchoma na kuvunja mabarabara kama ilivyotokea baada ya uchaguzi Mkuu mwaka huu kwani hali huliletea taifa hasara kubwa.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post