Kampuni ya mbolea nchini TFC imekabidhi mifuko ya mbolea katika halmashauri ya manispaa ya Ilemela ambayo itakabidhiwa katika shule mbalimbali wilayani humo lengo likiwa ni kuwawezesha kulima kilimo cha kisasa kitakachoongeza tija na mazao ya kutosha
Akizungumza wakati wa kupokea mbolea hiyo mkuu wa wilaya ya Ilemela AMIR MKALIPA ameishukuru TFC kwa msaada huo na kuongeza kuwa hii itakuwa ni chachu kwa wanafunzi kujifunza kilimo cha kisasa kitakachoweza kuwasaidia katika maisha yao ya baadae
Naye afisa masoko kutoka kampuni ya mbolea nchini TFC CLARA KABWE amesema lengo ni kuunga mkono jitihada za serikali na kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija pamoja na kuchochea suala la lishe kwa wanafunzi mashuleni
Post a Comment