Viongozi wa Taasisi za Kiislamu nchini wameonyesha wasiwasi wao kuhusu hatari ya kugawanyika kwa taifa na wamechukua msimamo wa kukemea vikali hila zote za kupandikiza chuki na uhasama kwa misingi ya kidini, kikabila, au kikanda.
Kauli hiyo waliitoa baada ya kukamilika kwa ibada ya Itikafu,chini ya Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir bin Ally.
Pamoja na mambo mengine tamko hilo limewaagiza Waislamu na viongozi wote wa dini nchini:
• Kukanya Jamii Dhidi ya Uovu: Dini zote nchini Tanzania zinapinga uhalifu, chuki, uharibifu wa mali na machafuko, hivyo viongozi wanapaswa kuhimiza kusameheana na mshikamano.
• Kukataa Hila za Fitina: Viongozi wa dini wameaswa kuzikataa hila za kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini na kuwaelimisha waumini wao juu ya hatari zake kwa umoja wa taifa.
• Kuunganisha Viongozi wa Dini: Taasisi hizo zimeagiza madawati yanayowaunganisha na wenzao wa dini nyingine kufanya haraka kuratibu mkutano wa viongozi wakuu wa dini kwa lengo la kuinusuru nchi na kuirejeshea amani yake.
Katika ibada hiyo Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir bin Ally, ametoa rai ya kutumia maneno na kauli za kujenga, za kuleta umoja na kuwa daraja kati ya Waislamu na kati ya Waislamu na Watanzania wengine wote. Wito huu unalenga kupunguza mvutano na kuimarisha mshikamano wa kitaifa ambao ulijengwa kwa miaka mingi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
✉️ info@eastafricanspirits.com
Post a Comment