" ATAKA KUJENGA SHULE YA SEKONDARI YENYE VIPAJI MAALUM

ATAKA KUJENGA SHULE YA SEKONDARI YENYE VIPAJI MAALUM



Na Mwandishi wetu, Misalaba Media

Diwan  wa Kata ya Nyanguku Jimbo la Geita Mjini, Elia Ngole amesema katika kipindi chake cha awamu ya tatu atahakikisha kuwa inajengwa sekondari kwa ajili ya wanafunzi wenye vipaji kuwezesha eneo hilo kupata vijana wasomi wa kutumainiwa.

Hayo amebainisha jana diwani huyo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika eneo hilo kuelezea mikakati yake baada ya ushindi aliopata katika uchaguzi uliokamilika mwezi wa Oktoba.

Alisema lengo la kuweka msukumo wa kufungua shule ya wanafunzi wenye vipaji ni kutaka kuinua kiwango cha elimu kwa watoto wa eneo hilo ili waweze kufikia matarajio ya kuwa wanataaluma wabobevu katika nyanja za Sayansi na Teknolojia.

"Natamani watoto wetu toka kwenye hii kata na wale walio karibu wasomi kwa bidii ili waweze kuwa na vipaji wajiunge tuweze kupata wanataaluma wazuri" alisema Ngole.

Alisema amefanikiwa kupata zaidi ya ekari 12 katika Kijiji cha Shinamwenda kwa ajili kuwezesha kujengwa kwa shule hiyo katika kata hiyo.

Aidha Ngole alisema kipaumbele chake kingine ni kwenye sekta ya usafirishaji ambapo ataendelea kuhamasisha wananchi kujitolea kwa nguvu kazi katika sehemu ambazo Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) watachelewa kutengeneza kuhakikisha kunapitika muda wote.

Alisema vilevile kipaumbele kingine ni kuhakikisha kuwa Kata inakuwa na kituo cha Afya ambapo tayari milioni 500 zimetengwa kuwezesha kata hiyo kuwa huduma hiyo ambapo kwa sasa wako kwenye hatua ya manunuzi.

📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post