Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Ndugu Jimotoli Jilala Maduka, amefanya kikao kazi na Makatibu wa Idara za Elimu, Malezi na Mazingira kwa lengo la kuimarisha utendaji na utekelezaji wa majukumu ya Jumuiya hiyo wilayani humo.
Kikao hicho kilifanyika tarehe 25 Februari 2026, kikilenga kujadili mikakati ya kuboresha sekta ya elimu, kuimarisha malezi kwa vijana pamoja na kusimamia masuala ya mazingira ndani ya Jumuiya na jamii kwa ujumla.
Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Jimotoli alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi wa idara hizo ili kuhakikisha malengo ya Jumuiya ya Wazazi yanafikiwa kwa ufanisi. Alieleza kuwa elimu na malezi bora ni msingi wa maadili mema kwa vijana, huku akihimiza utekelezaji wa programu zitakazochochea uwajibikaji na nidhamu kwa wanafunzi.
Kwa upande wa mazingira, kikao kilijadili namna ya kuhamasisha wanachama na jamii kushiriki katika shughuli za uhifadhi wa mazingira, ikiwemo kampeni za usafi, upandaji miti na utunzaji wa maeneo ya shule na ofisi za Jumuiya.
Makatibu wa idara hizo walipata fursa ya kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa majukumu yao pamoja na changamoto wanazokutana nazo, huku wakiahidi kuongeza juhudi katika kusimamia mipango iliyowekwa kwa manufaa ya Jumuiya na jamii ya Mpanda kwa ujumla.
Wakati huo huo Ndugu Jimotoli Jilala Maduka ameweka msisitizo mkubwa katika nidhamu ya kazi, uwazi wa mapato na matumizi ya miradi, pamoja na kuandaa mpango kazi wa pamoja kwa mwaka 2026 ili kuhakikisha Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mpanda inazidi kuwa imara kiutendaji na kiuchumi.
Kikao hicho kimeelezwa kuwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha uongozi wa karibu, kuongeza uwajibikaji na kuleta matokeo chanya ndani ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mpanda.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment