
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linafanya uchunguzi wa tukio la ajali ya gari kuwaka moto na kuteketea.
Tukio hilo limetokea asubuhi ya leo, Disemba 9 katika eneo la Maseyu kona kali, kata ya Gwata, wilaya ya Morogoro mkoani humo ambapo gari lenye namba za usajili T. 947 DVR aina ya Tata lililokuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam Kwenda wilaya ya Malinyi likiendeshwa na Halfan Omary, dereva na mkazi wa Mbezi Dar es Salaam likiwa na abiria 40 liliwaka moto na kuteketea.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ktika tukio hilo hakuna abiria aliyepata madhara licha ya mizigo na mali nyingine za abiria kuharibika na kuteketea kufuatia moto huo.
“uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya mifumo ya umeme wa gari hilo” taarifa hiyo imedokeza na kuongeza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea.
Kufuatia tukio hilo, Jeshi la polisi limewataka wamiliki wa vyombo vya moto kuwa na utamaduni wa kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya magari yao hasa yanayobeba abiria ili kuokoa maisha ya watu na mali.
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment