" BLOGU:TUMIENI BLOGU KUPATA MAARIFA

BLOGU:TUMIENI BLOGU KUPATA MAARIFA

Na: Mbeki Mbeki.

Kagera.

Blogu ni jukwaa la mtandaoni linalochapisha makala au maudhui mara kwa mara kuhusu mada maalum kama michezo,siasa,elimu au masuala ya kijamii.

 Hutofautiana na media za jadi kwakuwa na uhuru mkubwa wa mtindo na maoni lakini imekuwa chanzo muhimu cha taarifa kwa wasomaji wa kisasa.

Kwa jamii ,blogu zina faida nyingi huongeza elimu na maarifa,hutoa sauti kwa wananchi kueleza changamoto zao,na hukuza mijadala ya kijamii inayoweza kuleta suluhu.

pia,blogu huhamasisha mabadiliko ya kitabia,kuibua kampeini za kijamii ,na kuwa rejea ya kudumu ya taarifa na historia.

Ili blogu iaminike lazima izingatie maadili ya uandishi. 

Kanuni  muhimu ni ukweli na usahihi wa taarifa ,uwazi wa vyanzo,uwiano wa hoja bila  upendeleo,na uwajibikaji kusahihisha makosa .

Vile vile ,mwandishi anapaswa kuzingatia heshima na utu wa watu ,kuepuka upotoshaji na huzush na kutumia uhuru wa kuandika kwa namna ya kujenga badala ya kubomoa.

Blogu,isipozingatia maadili haya inaweza kueneza  taarifa za uongo ,chuki ,na taharuki hali inayoharibu uaminifu wa wasomaji na ustawi wa jamii kwa ujumla,blogu ni chombo cha maarifa na ushawishi chenye nguvu ,na uwajibikaji wa kimaadili ndio nguzo yake ya kuaminika.

Ili biashara yako iweze kuwafikia watu na wateja wako wengi zaidi  Tanzania na nje ya nchi👇 

📞 Wasiliana na Misalaba Media ili kuanza kushirikiana Rasmi

🌍 Tovuti: www.misalabamedia.com
📧 Barua pepe: misalabamedia@gmail.com
📞 Simu: 0745 594 231
📍 Makao Makuu: Shinyanga Mjini, Tanzania

 

Post a Comment

Previous Post Next Post