Na.Belnardo Constantine, Misalaba Media Chama cha Kitume cha Mtakatifu Egidio kutoka Kanisa Katoliki, kinachojumuisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali Jijini Dodoma kimefaraji wafungwa wa gereza kuu la isanga mkoani dodoma Kwa kutoa msaada wa msaada wa mahitaji muhimu kwa wafungwa Misaada hiyo litolewabtarehe 26/12/ kama zawadi ya sherehe za chrisimasiAidha Nduga Anthony Mdonyela, akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake wakati wa zoezi la makabidhiano hayo, alieleza kuwa msaada huo ni sehemu ya matendo ya huruma na faraja kwa wahitaji, hasa wafungwa waliopo magerezani. Alisisitiza kuwa ni mwendelezo wa maadili ya upendo na mshikamano yanayofundishwa na kanisa.Kwa niaba ya Mkuu wa Gereza Kuu Isanga, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza SSP. Joseph Mwambiga, amekishukuru chama hicho cha kitume cha Mtakatifu Egidio kwa moyo wa kujitolea, akisema msaada huo una mchango mkubwa katika kuwajenga kisaikolojia wafungwa. Alisisitiza kwamba msaada unawapa matumaini na kuwafanya waamini kuwa jamii inawajali na kuwakumbuka licha ya hali walizonazo.“Upendo na mshikamano muliouonesha leo hii ni msingi wa kuwajenga wafungwa na kuwapa matumaini mapya ya maisha bora baada ya vifungo.” aliongeza SSP. Mwambiga.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment