Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) imeendesha tamasha la kutoa elimu na furusa mbalimbali za uhifadhi jijini dar es salaam katika viwanja vya maonyesho ya sabasaba vilivyopo barabara ya kilwa jijini hapa Aidha TAWA imewataka Wananchi kuendelea "kumiminika" katika Viwanja vya SabaSaba Kilwa Road Jijini Dar es Salaam kwenye tamasha hilo la mwaka lilopewa Jina la funga mwak Kijanja na TAWA linaloendelea katika Viwanja hivyo mpaka Januari 05, 2026.Hata hivyo TAWA imewakaribisha Wananchi wote kujionea na kuburudika Sambamba na kuelimika na kujifunza mengi kuhusu Uhifadhi na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo chini ya Usimamizi wa taasisi ya TAWA.sanjari na kupata fursa ya kununua na kumilikishwa nyara za Serikali zikiwemo ngozi za Simba, Chui, Fisi na nyingine nyingi.Sambamba na hilo TAWA inaeleza kuwa Wananchi watapata furusa adimu ya kula nyama choma za wanyamapori mbalimbali na kupiga picha na taswira za wanyamapori wa aina mbalimbali na kubaki na kumbukumbu isiyosahaulika.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment