Na Lydia Lugakila, Misalaba Media MbeyaChuo cha Biblia cha Christian Evangelical (CEBI) mkoani Mbeya kimefanya Mahafali yake ya 21 kwa mwaka 2025 na kufanikiwa kuvuna wahitimu wa kwanza wa PHD wanne, pamoja na wahitimu wengine wa ngazi mbalimbali.Akizungumza katika mahafali hayo yaliyowakutanisha wahitimu kutoka matawi ya Tanzania na Malawi, Mkuu wa Chuo hicho Prof. Elnest Nguvila alisema kuwa chuo Cha CEBI kimeendelea kuzalisha vijana wenye maarifa na ujuzi utakaowawezesha kufanya kazi kanisani na katika jamii kwa ufanisi na kwa moyo wa kumtukuza Mungu.Nguvila amesema kwa mwaka huu wa 2025, kati ya wanafunzi 11 waliokuwa wakisoma shahada ya uzamivu (PHD), wanne ndio wamehitimu, huku wengine wakikosa kukidhi vigezo vya kitaaluma vinavyohitajika kutoka kwa wasimamizi wa ndani na nje ya nchi."PHD inahitaji maarifa makubwa Chuo chetu kinaongozwa na misingi ya utafiti wapo ambao hawajamaliza tafiti zao, na tunasisitiza ubora kwa ajili ya matokeo yenye tija kwa kanisa na jamii,” alisema Prof. Nguvila.Aidha, aliongeza kuwa wasomi wanaotafuta shahada ya uzamivu wanapaswa kuwa watu wanaolenga kutatua changamoto zilizo ndani ya jamii.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Biblia CEBI, DSO Gerald Mwaulesi, akizungumza kwa niaba ya uongozi wa chuo, aliwapongeza wahitimu wote kutoka Tanzania na Malawi na kuwasisitiza kuendelea kulitangaza neno la Mungu popote watakapokwenda.Naye Prof. Harlex Kanthiti kutoka Malawi, aliyewaweka wakfu watumishi hao, aliwataka kutumia hekima na maarifa katika kulitumikia kanisa na jamii.Naye mgeni rasmi katika mahafali hayo Askofu Bernard Mwalyego, alipongeza chuo hicho Kwa hatua hiyo huku akiwataka wahitimu kutokatishwa tamaa na mtu yeyote huku akiwatia moyo na kuwasihi wajione jinsi Mungu anavyowaona katika huduma yao."Watumishi wa Mungu wanatakiwa kujitambua wao ni nani katika huduma, na kuwa tayari kukabiliana na changamoto,” alisema Askofu Mwalyego.Kwa upande wao, baadhi ya wahitimu wa PHD akiwemo Godfrey Mwandumbya, Richard Mwaswala na Peter Benerd, walisema kuwa safari ya utafiti imekuwa ngumu lakini yenye mafanikio na kuwasihi wanaotamani kusoma PHD kutokata tamaa kwani inawezekana.
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

















































Post a Comment