Na Lydia Lugakila -Misalaba media
Missenyi
Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera inatarajiwa kuandika historia mpya baada ya kutangazwa rasmi kuanzishwa kwa Mashindano ya “Cocoa Cup”, yatakayofanyika kuanzia Julai hadi Oktoba 2026, yakishirikisha kata zote 20 za wilaya hiyo.
Mashindano hayo yanaratibiwa na Jonathan Jesse, yakilenga kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu kilimo cha Cocoa (Kakao) kama zao la kimkakati na lenye faida kubwa kiuchumi.
Dhamira ya Mashindano
Lengo kuu la Cocoa Cup ni kutangaza fursa za kilimo cha Cocoa kwa vitendo, kwa kutumia michezo, sanaa na utamaduni kama nyenzo ya kujenga uelewa, hamasa na motisha kwa wananchi wa Missenyi, hususan vijana na wanawake, ili wachangamkie kilimo hicho chenye tija.
Kwa mujibu wa Jesse Kata zitakazoshiriki
Mashindano ni kata zote 20 za Wilaya ya Missenyi ambazo ni: Bugandika, Bugorora, Buyango, Bwanjai, Gera, Ishozi, Ishinju, Kakunyu, Kanyigo, Kashenye, Kassambya, Kilimilile, Kitobo, Kyaka, Mabale, Minziro, Mushasha, Mutukula, Nsunga na Ruzinga.
Michezo na shughuli Zitakazoshindaniwa
Mashindano ya Cocoa Cup yatahusisha wanaume na wanawake katika michezo na shughuli zifuatazo:
mpira wa miguu
Ngoma za asili
Riadha (mbio za kukimbia)
Kuruka kamba / Kuguruka
Bao la asili (Olweso)
Matokeo yanayotarajiwa
Kupitia mashindano haya, Wilaya ya Missenyi inalenga
Kuongeza uelewa wa Wananchi kuhusu kilimo cha Cocoa,
Kuchochea ushiriki wa jamii katika kilimo cha kisasa
Kukuza vipaji vya michezo na utamaduni,
Kujenga mshikamano na umoja miongoni mwa kata za wilaya.
Mashindano ya Cocoa Cup yanatarajiwa kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku yakiiweka Missenyi katika ramani ya uzalishaji wa Cocoa nchini.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment