Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya amezitaka ofisi za Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kutoa taarifa ya kila mwaka kuhusiana na masuluhisho mbalimbali ya migogoro ya ardhi inayoshughulikia."Tuharakishe kushughulikia mashauri yaliyowekwa kwenye mabaraza ya ardhi na nyumba ya wilaya na tusikae na mashauri hayo bila sababu yoyote" amesema Mhe. Mmuya.Mhe. Mmuya ametoa kauli hiyo leo Desemba 16,2025 mkoani Lindi alipokutana na Watumishi wa Sekta ya Ardhi katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.Vilevile, Mhe. Kaspar Mmuya amewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kuhakikisha maeneo yaliyotambuliwa wananchi wake wanapatiwa hati milki ya ardhi."Tunataka kila mtanzania mwenye eneo ambalo limepimwa na limepangwa apewe hati yake".amesema Mhe. MmuyaAidha, amewataka Wataalamu wa sekta ya ardhi nchini kutekeleza kikamilifu maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Kuhakikisha kila kipande cha Ardhi kinapimwa.Amesema, dhamira ya Rais Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi itasaidia kuondoa changamoto za migogoro ya mipaka ikiwemo ile ya vijiji na vijiji.Kikao kazi baina ya Naibu Waziri Mmuya na Watumishi wa sekta ya ardhi kimelenga kutambua juhudi za watumishi wa sekta hiyo katika kutimiza malengo ya Wizara lakini pia kufahamu changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao .


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment