" MADEREVA WA MASAFA MAREFU WATAKIWA KUEPUKA MATUMIZI YA VILEVI ILI KUKATA USINGIZI

MADEREVA WA MASAFA MAREFU WATAKIWA KUEPUKA MATUMIZI YA VILEVI ILI KUKATA USINGIZI


Madereva wanaoendesha magari ya masafa marefu, hususan magari ya abiria, wamepewa elimu ya kujiepusha na matumizi ya vilevi nyakati za usiku kwa lengo la kukata usingizi.

Elimu hiyo imetolewa na askari Polisi wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, wakati akizungumza na madereva wa magari ya abiria. Amewataka madereva hao kutojihusisha na vitendo hivyo kwani matumizi ya vilevi husababisha uchovu, hupunguza umakini na yanaweza kusababisha dereva kushindwa kulimiliki gari, kupoteza uelekeo na hatimaye kusababisha ajali.

Kwa upande wao, madereva wamepongeza elimu hiyo wakisema imewasaidia kuelewa madhara ya matumizi ya vilevi wakati wa kazi, na kuahidi kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa manufaa yao na abiria kwa ujumla.

Post a Comment

Previous Post Next Post