" MBUNGE ATOA TAILI 4 ZA GARI KWA JESHI LA POLISI

MBUNGE ATOA TAILI 4 ZA GARI KWA JESHI LA POLISI


 Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media

 Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Mhe. Deo Mwanyika amekabidhi taili 4 za gari zenye thamani ya shilingi milioni 2.214 kwa Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe.

 Taili hizo zimekabidhiwa Leo tarehe 11,Disemba 2025, Kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi Mahamoud Hassan  Banga,  ikiwa ni  sehemu ya mchango wa Mh. Deo Mwanyika  Ambaye ni mbunge  wa jimbo hilo  Kwa lengo kuunga mkono juhudi za jeshi la polisi  katika kuimarisha ulinzi na usalama.

Aidha makabidhiano  hayo yamefanyika kupitia kwa Katibu  wa Bunge  Bw. Chrispin Kalinga, ambaye alimwakilisha Mbunge Mwanyika katika hafla hiyo fupi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Bw. Kalinga alisema kuwa Mbunge Mwanyika ametoa vifaa hivyo baada ya kutambua mchango mkubwa wa Jeshi la Polisi katika kuhakikisha wananchi wa Njombe wanaishi katika mazingira salama.

“Kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Mhe. Deo Mwanyika, napenda kusema kuwa msaada huu ni ishara ya kuthamini kazi kubwa na ya kujitolea ambayo Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linaifanya kila siku. Mhe. Mwanyika ametambua juhudi zenu za kulinda amani, usalama wa raia na mali zao, na ameona ni muhimu kuyaunga mkono mazingira yanayowawezesha kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi zaidi,”

 alisema Kalinga katika hafla hiyo .

Hatahivyo upande Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe Wakiwakilishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani hapo  limetoa  shukrani za dhati kwa Mbunge Mwanyika kwa hatua yake ya kuonyesha ushirikiano na kuthamini kazi ya vyombo vya ulinzi na usalama.

 “Napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Mhe. Deo Mwanyika, kwa kutambua na kuthamini kazi inayofanywa na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha wananchi wa Njombe wanaishi kwenye mazingira salama. Msaada huu wa taili za gari unarahisisha utendaji kazi wetu na unaonyesha namna viongozi wa eneo letu wanavyoliona suala la usalama kama ajenda ya msingi ya maendeleo,” alisema kamanda Banga.

Aidha, aliongeza kuwa Jeshi hilo litaendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujituma ili kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kupatikana katika mkoa wa Njombe.

 “Tunamshukuru sana Mheshimiwa Mwanyika kwa moyo huu wa upendo. Tunathamini mchango wake, kwani utasaidia kulinda raia na Mali zao.


📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post