MSHAGATILA AAPISHWA RASMI DIWANI WA KATA YA KOLANDOTO: MWANZO MPYA WA MAENDELEO KATA YA KOLANDOTO
Officialgamaya0
Na Elias Gamaya -SHINYANGA
Diwani mpya wa Kata ya Kolandoto katika Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Mshagatila Moses Kashinje, ameapishwa rasmi
leo Desemba 04, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwl. Alexius
Kagunze, Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza mara baada ya kuapishwa, Mhe. Mshagatila
ameahidi kushirikiana kwa karibu na wananchi, viongozi wa mitaa pamoja na
watumishi wa Halmashauri katika kutatua changamoto zinazoikabili Kolandoto,
akisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi ndiyo kipaumbele chake kikuu.
Kuapishwa kwa Mhe. Mshagatila kunafungua ukurasa mpya wa
uongozi katika kata hiyo, ambapo wananchi wanatarajia kuona kasi mpya ya
maendeleo, uwajibikaji ulio imara na utatuzi wa changamoto zinazowakabili
katika maisha yao ya kila siku.
Post a Comment