Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa onyo kali na la mwisho kwa watu wanaojiita wanaharakati na "vibaraka" wa mataifa ya nje, ambao wamekuwa wakieneza uzushi wa kutisha kuhusu idadi ya vifo vilivyotokea wakati wa vurugu za hivi karibuni.
Akizungumza na maelfu ya wananchi wa Tunduma mkoani Songwe wakati wa ziara ya kukagua madhara ya vurugu za Oktoba 29, Dkt. Mwigulu amewashangaa watu wanaofurahia "kuhesabu miili" ya Watanzania kwa ajili ya kujipatia fedha kutoka kwa wafadhili wao ughaibuni.
Uzushi wa "Vifo Elfu 10": Hoja ya Kitoto na Hatari
Dkt. Mwigulu amepasua jipu kuhusu takwimu zinazosambazwa na wachochezi hao wanaodai kuwa maelfu ya watu wamepoteza maisha, akibainisha kuwa madai hayo ni ya kipumbavu na yanalenga kuipaka matope Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Wanatamani wahesabu miili ili wapate fedha nyingi zaidi. Wameng'ang'ana kusema watu elfu 10 wamekufa. Hivi unajua maana ya watu elfu 10? Unacheza na damu ya watu elfu 10?" alihoji Dkt. Mwigulu kwa hasira na kuongeza: "Watu elfu 10 wamwagike kwa mapigano halafu ardhi iwe nyeupe tu? Huku ni kutafuta laana!"
Vibaraka Waliotumwa Kuchochea Ghasia
Waziri Mkuu ameweka wazi kuwa Serikali inafahamu michezo yote inayofanywa na watu wanaolipwa ili kuanzisha vurugu nchini. Amebainisha kuwa wanaharakati hao wanatumia maisha ya Watanzania masikini kama mtaji wa biashara yao ya kisiasa huku wao wakiwa wamejificha kwenye usalama.
"Wapo wanaharakati wanaolipwa kwa ajili ya kufanikisha kuchochea vurugu nchini. Wanatamani kuona nchi inapata ghasia ili wapate cha kuripoti kwa waliowatuma. Jambo hili halikubaliki na halitavumiliwa hata kidogo," alisisitiza Waziri Mkuu.
Dkt. Mwigulu amehitimisha kwa kuwatoa hofu Watanzania na kuwaahidi kuwa Serikali itapambana na yeyote atakayejaribu kuchezea amani ya nchi. Amewataka wakazi wa maeneo ya mipakani kama Tunduma kuwa macho na watu wanaoingiza chuki kwa kisingizio cha kutetea haki, huku lengo lao likiwa ni kudhoofisha nchi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment