" RC MTAMBI AWATAKIA WANANCHI WA MARA HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA, AHIMIZA AMANI NA USALAMA SIKUKUU

RC MTAMBI AWATAKIA WANANCHI WA MARA HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA, AHIMIZA AMANI NA USALAMA SIKUKUU

 Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 24 Disemba, 2025 amezungumza na Waandishi wa Habari na amewatakia wananchi wa Mkoa wa Mara heri ya sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya, 2026. 

Mhe. Mtambi amewahakikishia wananchi kuwa Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara imejipanga kuhamasisha Mkoa unakuwa salama wakati na baada ya sikukuu. 

Mhe. Mtambi amewataka madereva wa vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani na kutumia muda huu wa sikukuu kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika Mkoa wa Mara. 

Aidha, Mhe. Mtambi ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa Mkoa wa Mara kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi cha mwaka mzima na kuwataka kuendelea kudumisha amani na utulivu wakati wote.

Post a Comment

Previous Post Next Post