Katika hatua inayoonyesha wazi kuwa Serikali imesikia na kujibu mahitaji ya haraka ya vijana (maarufu kama 'Gen Z') kuhusu elimu, ujuzi, na ajira, Wizara Kuu kadhaa zimekutana Dodoma kuweka mikakati thabiti.
Lengo kuu la mkutano huo lilikuwa kuimarisha ushirikiano ili kuwawezesha vijana wa Tanzania kupata fursa zinazokidhi mahitaji ya soko la ajira na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.
Kikao hicho kilijumuisha ushirikiano mkubwa kutoka:Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana.
Kikao hicho kiliwekewa msukumo na viongozi waandamizi, wakiongozwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo, na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Jenifa Omolo.
Profesa Nombo alisisitiza jinsi Serikali inavyotumia mifumo yake rasmi kujibu changamoto za vijana kuhusu ujuzi: Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014, Toleo la 2023, pamoja na mitaala iliyoboreshwa, vinaendelea kumwandaa kijana wa Kitanzania kupata ujuzi unaohitajika katika ulimwengu wa kazi.
Sera hiyo inatoa nafasi hata kwa vijana walioacha shule awali kurejea na kupata elimu kupitia mfumo rasmi na usio rasmi.
Aidha Serikali inaendelea kupanua fursa za ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, kutoa mikopo ya elimu, pamoja na ufadhili kupitia Samia Scholarship ili kuongeza wigo wa vijana kupata elimu na ujuzi.
Katibu Mkuu, Jenifa Omolo, aliipongeza Wizara ya Elimu kwa kuanzisha programu hizi zinazolenga kuwawezesha vijana kujitegemea na kushindana katika soko la ajira, akisisitiza kuwa programu hizo ni muhimu kuchochea ushiriki wa vijana katika uchumi wa taifa.
Maazimio Makuu ya Ushirikiano
Ili kuhakikisha vijana wanapata taarifa sahihi na kuunganishwa moja kwa moja na soko la ajira, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha maeneo yafuatayo:Upatikanaji wa taarifa,rasilimali fedha na ushirikiano wa viwanda.
Kuimarisha upatikanaji wa taarifa za fursa kwa vijana,Kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kugharamia mafunzo mahususi na stadi za kisasa na Kuratibu programu zitakazowaunganisha vijana na viwanda ili kupata mafunzo kwa vitendo (practical training) kumeelezwa ndio hitaji la haraka la vijana kwa sasa.
Kikao hiki kinatoa ishara wazi kwamba Serikali inatambua mchango mkubwa wa vijana na imedhamiria kuondoa vikwazo vinavyokwamisha upatikanaji wao wa elimu bora na ajira.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment