Na Lydia Lugakila, Misalaba Media – Bukoba
shule ya kiislamu ya Qudus Msingi na Sekondari iliyopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera imetangaza rasmi nafasi za masomo kwa mwaka 2026, huku uongozi wa shule hiyo ukitangaza ofa kabambe ikiwemo kupunguza ada ili kuwawezesha wazazi na walezi kuwasomesha watoto wao katika mazingira bora zaidi.
Akizungumza na vyombo vya habari, Bw. Shakiru Kalembalemba, mmoja wa viongozi wa shule hiyo, amesema wameamua kuja na ofa hiyo kama njia ya kusaidia jamii Ili watoto wapata elimu bora kwa gharama nafuu, sambamba na kuboresha malezi na usalama wa wanafunzi.
Shule hiyo yenye kutwa na bweni kwa wavulana na wasichana inapatikana Manispaa ya Bukoba, Mkoani Kagera, eneo la Rwazi–Kahororo, na imekuwa ikitambulika kwa mazingira tulivu, miundombinu rafiki kwa wanafunzi, pamoja na nidhamu ya hali ya juu.
Bw. Kalembalemba ameeleza kuwa ada kwa bweni imeshuka kutoka Sh 1,800,000/= hadi Sh 1,400,000/= kwa mwaka, hatua inayolenga kupunguza mzigo kwa wazazi na walezi.
Aidha, ada ya kutwa ni Sh 960,000/=, huku bweni likibaki Sh 1,400,000/= kwa mwaka.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa shule hiyo imejipambanua kwa kuwa na Maabara kamili za sayansi
Walimu wenye uzoefu, mazingira salama na tulivu,
ufaulu mzuri kila mwaka kwa darasa la nne, la saba, kidato cha pili na cha nne
Ameongeza kuwa shule hiyo inatoa elimu ya dini inayowajenga wanafunzi kuwa waadilifu, wema na wenye maadili ya Kiislamu, sambamba na utekelezaji wa elimu ya darasani.
Amehitimisha kwa kuwataka wazazi na walezi ndani Mkoa wa Kagera na nje ya mkoa huo kuiamini shule ya kiislamu Qudus ni chaguo sahihi la kuwapatia watoto wao elimu bora na mazingira salama ya kujifunza.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254









Post a Comment