Na Fabius Clavery, Misalaba Media-Kagera.Umoja wa Wahaya,Bukoba Homeland(BHL) umeiomba Serikali ya Mkoa wa Kagera kuwapatia eneo maalum kwa ajili ya kutekeleza shughuli za uwekezaji zitakazosaidia kuimarisha uchumi wa wanachama wake.Ombi hilo limetolewa na Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, Philbert Pantaleo, wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa umoja huo uliofanyika Desemba 27, 2025 jijini Bukoba.Pantaleo amesema umoja huo, ulioanzishwa mwaka 2021, umekuwa ukifanya shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa lengo la kuinua hali za maisha ya wanachama wake pamoja na kushiriki katika matendo ya huruma kwa jamii, hususan kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum.Kwa upande wake, mgeni rasmi katika mkutano huo, Ajes Katumwa, Afisa Tawala wa Wilaya ya Bukoba, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatuma Mwassa, amepongeza juhudi za umoja huo kwa kuendeleza mshikamano, kufanya matendo ya huruma katika jamii pamoja na kudumisha utamaduni wa “kukumbuka nyumbani”.Ameeleza kuwa kuhusu ombi la eneo la uwekezaji, umoja huo unaweza kupatiwa eneo baada ya kubainisha mahitaji yao ya uwekezaji na kuainisha halmashauri husika, kisha kuwasilisha maombi rasmi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.Kadhalika, Katumwa amewataka maafisa maendeleo mkoani Kagera kuweka utaratibu wa kutembelea vikundi vya kijamii na kiuchumi kama Bukoba Homeland ili kuvishauri juu ya namna bora ya kukuza mitaji yao, ikiwemo fursa za kupata mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri.Awali, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Kagera Faris Buruhan, ameahidi kuendelea kushirikiana na umoja huo nyakati zote watakapohitaji ushirikiano wake katika shughuli zao mbalimbali.Bukoba Homeland ni kikundi kinachojumuisha vijana 225 wazawa wa Mkoa wa Kagera wanaoishi katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania, kikilenga kuimarisha mshikamano, uchumi na maendeleo ya kijamii.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







Post a Comment