" ASKOFU CHINYONG’OLE AONGOZA IBADA YA KIPAIMARA NA KUMSIMIKA MCHUNGAJI MARGARETH NDONDE KANISA LA MT. ANDREW - SHINYANGA

ASKOFU CHINYONG’OLE AONGOZA IBADA YA KIPAIMARA NA KUMSIMIKA MCHUNGAJI MARGARETH NDONDE KANISA LA MT. ANDREW - SHINYANGA

Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, Mhashamu Johnson Japheth Chinyong'ole, amewawekea mikono wanafunzi 26 wa Kipaimara kutoka makanisa ya Mtakatifu Andrew Kitangili, Iwelyangula, Kizumbi na Busongo, katika ibada maalum iliyofanyika leo Desemba 28, 2025 katika Kanisa la Mtakatifu Andrew Kitangili, Mkoani Shinyanga.

Zoezi hilo limehitimisha safari ya mafundisho ya Kipaimara iliyoanza mwezi Septemba mwaka huu, ambapo vijana hao walipokea mafundisho kuhusu imani, maadili na uwajibikaji wa Kikristo.

Akizungumza katika ibada hiyo, Askofu Chinyong'ole aliwasihi vijana waliopewa Kipaimara kuendelea kuishi kwa kutenda matendo yanayoakisi mafundisho waliyopata, huku akisisitiza kuwa Kipaimara ni hatua ya kuonesha ukomavu wa kiroho.

“Ninawaomba muweke moyoni kile mlichofundishwa. Kipaimara si mwisho wa safari, bali ni mwanzo wa kutembea kwa imani. Jiepusheni na mambo ya kidunia yanayoharibu tabia na maadili; wekeni alama ya kiroho katika maisha yenu kwa sala, kumtumikia Mungu na kuheshimu wazazi wenu,” amesema Askofu. Chinyong'ole

Katika hatua nyingine vijana hao wameaswa kushiriki kikamilifu katika shughuli za Kanisa na kujitolea kwa ajili ya huduma za kijamii, akisema hilo ndilo linalothibitisha matunda ya Kipaimara.

“Kanisa linahitaji vijana wenye msimamo na utu. Msirudi nyuma. Endeleeni kusoma Neno la Mungu, kuwa watu wa maombi na kuepuka vishawishi vinavyowapoteza,” aameongeza Askofu Chinyong'ole.

Kwa upande wake, Mchungaji wa Kanisa la Mtakatifu Andrew Kitangili Joan Ndabakubije, amewapongeza wana Kipaimara hao na kueleza kuwa tukio hilo limeandika historia muhimu kwa Kanisa hilo.
“Leo ni siku ya furaha kwa Kanisa letu. Tumeshuhudia kizazi kipya kinachojengwa katika imani na maadili. Tunaamini mtakuwa mfano bora katika jamii na Kanisa litaendelea kusimama imara kupitia ninyi,” amesema Mchungaji Ndabakubije.

Mbali na tukio hilo katika ibaada hiyo maalumu imeenda sambamba na kusimikwa kwa Dkt. Margareth Aidan Ndonde kuwa Mchungaji shemasi katika Dayosisi ya Shinyanga, ambaye pia ni katibu wa UMAKI, anayeratibu Shughuli za maendeleo ya wanawake na Watoto taifa


Mhashamu Johnson Japheth Chinyong'ole Akizungumza katika ibada maalumu ya kipaimara kwa wanafunzi 26 hafla iliyofanyika katika kanisa la Anglikani Mtakatifu Andrew Kitangili

Mchungaji wa Kanisa la Mtakatifu Andrew Kitangili Joan Ndabakubije, akizungumza katika ibaada                                                              hiyo maalimu ya kipaimara



























 

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post