Na Fabius Clavery, Misalaba Media-Kagera Waziri wa Kilimo na Uvuvi, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amewataka wadau wa uvuvi mkoani Kagera kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria, hatua itakayowezesha wawekezaji kupata malighafi bora na endelevu.Wito huo umetolewa Desemba 29, 2025, wakati wa mkutano wa wadau wa uvuvi uliofanyika wilayani Muleba, mkoani Kagera.Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Kakurwa amesema kwa kipindi kirefu kumekuwepo na uvunjifu wa sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya uvuvi nchini, hususan matumizi ya nyenzo zisizokidhi viwango.“Kwa muda mrefu tumeshuhudia ukiukwaji wa sheria na kanuni za uvuvi, ikiwemo matumizi ya zana sisiOkidhi vigezo ambazo zinahatarisha uendelevu wa rasilimali za uvuvi nchini,” amesema Dkt. Kakurwa.Aidha, Waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kulinda samaki wazazi ili kuhakikisha rasilimali za uvuvi zinaendelea kuwepo kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa Malighafi za kutosha na zinazokidhi vigezo, akiwataka wavuvi kurejesha ziwani samaki wazazi watakaovuliwa kimakosa.“Ni muhimu sana kuwalinda samaki wazazi. Endapo watavuliwa kimakosa, wahakikishe wanarudishwa ziwani mara moja ili kulinda mazalia ya samaki,” ameongeza.Katika hatua nyingine, Dkt. Kakurwa amewataka wavuvi kujiepusha na biashara ya nyavu haramu, huku akiziagiza mamlaka husika kudhibiti kwa nguvu zote uingizaji wa nyavu zisizokidhi viwango nchini.Vilevile, amewataka wamiliki wa viwanda vya kuchakata samaki kuacha mara moja tabia ya kupeleka mitumbwi kwenye visiwa kwa ajili ya kuvua samaki, akionya kuwa yeyote atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufutiwa leseni.“Hakuna mmiliki wa kiwanda atakayeruhusiwa kupeleka mitumbwi visiwani kwa ajili ya kuvua. Atakayekiuka, hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufutiwa leseni,”amesisitiza Waziri huyo.Awali, baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wameiomba serikali kusimamia kikamilifu sheria za uvuvi, na wakisema hatua hiyo itasaidia kudhibiti uvuvi usiofaa na kuongeza mazalia ya samaki katika Ziwa Victoria.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment