" Waziri wa Ulinzi wa Jeshi la kujenga Taifa afanya ziara ya Kikazi Makao ya JWTZ

Waziri wa Ulinzi wa Jeshi la kujenga Taifa afanya ziara ya Kikazi Makao ya JWTZ



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho (Mb) tarehe 05 Desemba 2025, amefanya ziara ya Kikazi kutembelea Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Msalato Dodoma kwa ajili ya kuzungumza na kujitambulisha kwa  Maafisa, Askari pamoja na Watumishi wa  Umma wa Makao Makuu ya Jeshi. 



Mara baada ya Kuwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi, Mhe Dkt. Rhimo alipokelewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda aliyeongoza Maafisa na Askari pamoja na watumishi wa umma kumlaki Waziri wa Ulinzi na JKT, na baadaye kuzungumza na Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma waliohudhuria hafla hiyo ya kumlaki Waziri wa Ulinzi na JKT Makao Makuu ya JWTZ 

Katika Hotuba yake, Waziri Nyansaho amemuhakikishia Mkuu wa Majeshi utayari wa Serikali ya Awamu ya Sita,inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha  Jeshi la Wananchi wa Tanzania linaendelea kuwezeshwa ili liendelee kutimiza Majukumu yake  ya Ulinzi wa Taifa. Waziri Rhimo akawaambia Maafisa na Askari wa JWTZ kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa JWTZ  na taasisi zake  kufikia malengo yanayokusudiwa.





Ziara ya Kikazi ya Waziri wa Ulinzi na JKT katika Makao Makuu ya JWTZ Msalato, ilihudhuriwa pia na Maafisa Jenerali, Maafisa wakuu, Maafisa na Askari pamoja na Watumishi wa umma.

📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post