" WIMBI LA UZALENDO MITANDAONI: WANANCHI WATETEZI WA AMANI NA MSHIKAMANO WA TAIFA

WIMBI LA UZALENDO MITANDAONI: WANANCHI WATETEZI WA AMANI NA MSHIKAMANO WA TAIFA

Wimbi kubwa la hasira na uzalendo limeendelea kutawala katika mitandao ya kijamii, hususan Instagram, ambapo maelfu ya wananchi wameibuka kupinga kile wanachokiita "ushetani na tamaa ya madaraka" inayolenga kuivuruga Tanzania. 

Hali hii inakuja baada ya kusambaa kwa video na kauli zinazodaiwa kuchochea uvamizi wa kijeshi na machafuko nchini, jambo ambalo Watanzania wameliandama kwa maneno makali.

Kwenye maoni yaliyofurika mtandaoni, wananchi wameonyesha kuchoshwa na harakati za watu binafsi na makundi yanayotumia mwamvuli wa dini na siasa kuvunja utulivu wa nchi. 

Mmoja wa watumiaji wa Instagram ametoa ujumbe mzito akisema, "Amani yetu ni nguzo yetu," huku wengine wakihoji dhamira ya wale wanaoomba nchi ivamiwe, wakisema: "Sijui hawa watu wanataka nini, ushetani unaowaingia hawajui madhara yake."

Mjadala huo haujawaacha salama viongozi wa dini na vyama vya siasa vinavyotajwa kuhusika na harakati hizo. Wananchi wengi wameelekeza lawama kwa Padri Kitima na baadhi ya washirika wa vyama vya upinzani, wakidai kuwa wamejificha kwenye kivuli cha "kudai haki" ili kutimiza matamanio yao ya madaraka. 

"Wanadai haki kivuli cha maovu yao, wanataka madaraka hawa tamaa inawasumbua," aliandika mdau mwingine.

Hisia za wananchi zimeonyesha kuwa Watanzania wa leo wameerevuka na hawako tayari kutumika kama daraja la machafuko. Wengi wamesisitiza kuwa yeyote anayeota kuona damu ikimwagika nchini anapaswa kukabiliwa kwa mkono wa chuma wa sheria.

 Kuna waliokwenda mbali zaidi na kusema, "Waunde tu kundi la uasi wauawe kihalali," ikionyesha kiwango cha juu cha uchungu walionao wananchi dhidi ya wanaotaka kuharibu amani iliyodumu kwa miongo mingi.

Licha ya presha na hamasa za hapa na pale, kauli mbiu iliyotawala ni moja: Tanzania ni nchi ya amani na tuko nyuma ya Rais wetu. Wananchi wametoa onyo kuwa michezo yoyote ya kitoto inayolenga kuyumbisha uchumi na usalama wa nchi haitafanikiwa, kwani "Amani ni ngao ya nchi yetu na tuilinde kwa gharama yoyote."

Post a Comment

Previous Post Next Post