Maafisa usafirishaji maarufu kama boda boda Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuacha mara Moja vitendo vya kutoboa eksozi kwenye pikipiki zaoAkitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaeleza kuwa vitendo hivyo vinasababisha kelele na milipuko mikubwa kutoka kwenye pikipiki hizo kitu ambacho kinapelekea kuhatarisha maisha Kwa watu wengine hususani wenye changamoto za kiafya kama magonjwa ya moyo na mengineyo.Sajenti Ndimila amewataka maafisa usafirishaji hao kutoa ushirikiano Kwa kupinga vikali vitendo hivyo Kwa kupeana elimu wao Kwa wao lakini pia kutoa taarifa ya wale wote wanaondelea kukaidi ili waweze kubainika Kwa urahisi na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.Kwaupande wao Maafisa usafirishaji hao wamelipongeza Jeshi la Polisi Kwa kutoa elimu hiyo na kuahidi ushirikiano wa dhati kutokomeza vitendo hivyo ambavyo vinaleta picha mbaya katika jamii.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment