" BANK OF AFRICA TANZANIA YATOA MAFUNZO YA FEDHA KWA WAJASIRIAMALI DAR

BANK OF AFRICA TANZANIA YATOA MAFUNZO YA FEDHA KWA WAJASIRIAMALI DAR

‎Dar es Salaam, Tanzania- Bank of Africa Tanzania yawapa mbinu mpya wafanyabishara wa kati na waodogo jinsi ya kupanua wigo wa biashara , matumizi , elimu ya fedha , uwekezaji wa kimkakati ili kusaidia ukuaji wa biashara zao nchini.‎Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika mafunzo hayo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo , Bw Hamza Cherkaoui alisema kwamba sekta ya SME ina mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa Tanzania , utoaji wa ajira na kuboresha maisha ya watu wenye kipato cha kati na kidogo.‎“Takribani wafanyabiashara na wajasiriamali 100 wamehudhuria mafunzo haya ya elimu ya fedha na kupata mbinu za kuweza kuvuka changamoto na vikwazo vyao vya kibiashara kwa kupata mafunzo kutoka kwa wataalamu wa fedha waliobobea,” ‎Aliongeza kwenye mafunzo hayo wanapata fursa na nafasi ya kukutana na kupanua wigo wa mtandao wa ushirikiano wa kibiashara na kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao kwa kupata fursa za majukwaa mapya ya biashara.‎“tuna matawi sehemu mbalimbali za Africa , kuanzia Kigali, kampala , Lubumbashi na sehemu zingine na ni muhimu ukienda kufanya biashara huko mnaweza kutembelea matawi yetu na kuongeza wigo wa ushirikiano wafanyabiashara wa nchini hizo na kufungua fursa zingine za biashara Afrika Mashariki,” alisema Bw Cherkaoui ‎Alisema kwamba Bank of Africa itaendelea kutoa mafunzo na ushirikiano na wafanyabiashara na wajasiriamali hapa nchini ili kuhakikisha kwamba wanakua pamoja katika kuboresha na kukuza uchumi wa nchini na mtu mmoja mmoja kwa kufanya biashara kwa ufanisi.‎Kwa upande wake , Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa kati na Wadogo (SME) , Bi Beatrice Richard alisema kwamba wafanyabiashara waliopata mafunzo hayo wanatoka kwenye sekta tofauti kama vile usafirishaji , kilimo, vyakula , vifaa vya umeme, ujenzi na sekta ya fedha katika Mkoa wa Dar es Salaam,‎“Umuhimu wa kuendesha mafunzo haya ya fedha na biashara kwa wafanyabiashara wa kati na wadogo ni kuwasaidia kupanua uelewa wao uhusu maswala ya fedha , kodi na na jisni ya kupata masoko mapya ili kukuza mapato yao,” alisema Bi Beatrice ‎Alifafanua kwamba katika kauli mbiu ya “kukua Pamoja” ni juhudi za benki katika kuhakikisha kwamba uelewa biashara kwa wafanyabiashara unaongezeka , jinsi ya kuweka akiba na mbinu za kuja na bidhaa mpya sokoni.‎Naye mfanyabiashara ambaye alihudhuria mafunzo hayo , Ndugu Kahlan Mazrui alisema kwamba mafunzo ni muhimu wa wafanyabiashara kwa sababu inaongeza uelewa wa matumizi ya fedha na maswala ya kodi na jinsi ya kuzungumza na wateja ili kukuza biashara zao.‎“Mimi ni Mkurugenzi wa Sokoni Microfinanc kupitia benki hii nimeweza kuwa na matawi 28 ya biashara ya ukopeshaji fedha kwa wajasiriamali wadogo wadogo na wajane hapa nchini ni hatua kubwa sana nimeipiga,” alisema ‎Pamoja na mambo mengine mafunzo haya yalikuwa ni fursa adhimu kwa wafanyabiashara kupata nafasi ya kujifunza namna bora ya kuzungumza na wateja na uanzishwaji wa bidhaa na uelewa mahitaji ya soko husika, Aliongeza Mazrui ‎Meneja wa Tawi Jipya la Lumumba la Bank of Africa Tanzania, Bi Gloria Victor alisema kwamba ni muhimu kwa wafanyabiashara kupata mafunzo ya fedha , mikopo na aina ya uwekezaji ambao unafaa.‎Alisema kwamba Bank of Africa Tanzania wamefungua tawi jipya la Lumumba ili wajasiriamali na wafanyabiashara kupata huduma za kifedha na mikopo kwa karibu zaidi.‎Bank of Africa Tanzania wamejikita katika kuhakikisha wanawapatia wajasiriamali wadogo na wa kati maarifa, nyenzo na masuluhisho ya kifedha wanayohitaji ili kustawi. ‎Kupitia programu kama SME Clinic, wanajenga ushirikiano endelevu na wa kudumu na wateja wao Kwa kauli mbiu ya , “Kuwezesha Ukuaji Pamoja” , wanadhihirisha dira yao ya kuwa mshirika wa kifedha anayeaminika anayekua sambamba na wateja wake  na sekta ya biashara  za Tanzania.‎Warsha n mafunzo kama hayo hufanyika kila mwaka na  ikisisitiza dhamira yake ya utoaji wa elimu ya masuala ya kifedha inayo lenga kuwawezesha wajasiriamali na kusaidia ukuaji wa biashara zao nchini kote.‎SME Clinic ni sehemu ya Programu ya Elimu ya Fedha ya Bank of Africa Tanzania , iliyoanzishwa mwaka 2021 kufuatia Kanuni za Ulinzi wa Watumiaji wa Huduma za Fedha za mwaka 2019. Kifungu cha 19 cha kanuni hizo kinahitaji kila mtoa huduma za kifedha kuandaa programu za elimu ya fedha kwa wateja wake. ‎Tangu ilipoanzanishwa programy hii, Bank of Africa Tanzania  imefanikiwa kuendesha warsha hizi (SME Clinics) mikoa ya  Dar es Salaam , Mwanza na Kahama na tayari imeweza kuwafikia zaidi ya wateja 800. ‎Kwa kauli mbiu ya mwaka huu  “ukuaji wa Pamoja”  SME Clinic inaendelea kutimiza malengo makuu ya benki yakiwemo, Kuunga mkono agenda ya Bank of Africa Tanzania  ya maendeleo endelevu hasa ahadi  yake namba 5, Kuhamasisha maendeleo ya watu kila maeneno na katika kutimiza Kanuni za Ulinzi wa Watumiaji wa Huduma za Fedha ya mwaka 2019.‎Mafunzo hayo yanalenga kuboresha ujuzi katika usimamizi wa biashara kwa wateja, Kuimarisha uhusiano kati ya Bank of Africa Tanzania  na wateja wake, na Kuhimiza matumizi ya mifumo na teknolojia za kidijitali ili kuongeza ufanisi wa biashara.‎Kuhusu Bank of Africa (T) Limited‎BANK OF AFRICA – TANZANIA ni benki ya kibiashara binafsi inayofanya shughuli zake nchini Tanzania kwa kuhudumia wateja wakubwa, wateja wadogo na wa kati pamoja na wateja wa rejareja. Ilianza rasmi nchini Tanzania mwezi Juni 2007 baada ya kununua Eurafrican Bank ambayo ilikuwa inafanya kazi tangu Septemba 1995. BANK OF AFRICA – TANZANIA ni sehemu ya BANK OF AFRICA GROUP ambayo ilianzishwa mwaka 1982 nchini Mali.‎BANK OF AFRICA GROUP ni kundi la kibenki la kimataifa barani Afrika, likifanya kazi katika nchi 18 za Afrika ikiwemo Afrika Magharibi, Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, na pia ina ofisi Paris, Uhispania, London (Uingereza) na China. Tangu mwaka 2010, BANK OF AFRICA imekuwa kampuni tanzu inayomilikiwa kwa kiwango kikubwa na BMCE Bank, benki ya tatu kwa ukubwa nchini Morocco, yenye uwepo katika nchi 31 na mabara manne.‎Kwa sasa, BANK OF AFRICA – TANZANIA ina matawi 17 ikiwemo 8 jijini Dar es Salaam na 9 katika mikoa mingine kama Arusha, Mwanza, Zanzibar na miji mingine mikuu.‎Mwisho

  

Post a Comment

Previous Post Next Post