Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alfred Mregi, amesema kuanzishwa kwa mfumo mpya wa kisasa wa ukusanyaji wa kodi unaojulikana kama Integrated Domestic Revenue Administration System (IDRAS) kutaleta mapinduzi makubwa katika usimamizi wa kodi za ndani na kuongeza uwazi katika shughuli za biashara nchini.Akizungumza leo Januari 21, 2026 jijini Dar es Salaam, Mregi amesema TRA imepanga kuunganisha jumla ya taasisi 300 kwenye mfumo huo, hatua itakayopanua wigo wa kodi na kurahisisha ulipaji kwa walipakodi.Mregi amesema katika awamu ya kwanza, kampuni 60 zitaunganishwa na mfumo huo, akisisitiza kuwa IDRAS ni rafiki kwa mtumiaji na una uwezo wa kuchakata taarifa kwa haraka, hivyo kupunguza muda na gharama kwa wafanyabiashara.“Mfumo huu ni rafiki kwa mtumiaji, unachakata taarifa kwa haraka na utaondoa changamoto zilizokuwepo awali. Pia utasaidia kuongeza uwazi na kuondoa vishoka katika masuala ya kodi,” amesema Mregi.Ameongeza kuwa TRA imejipanga kuhakikisha walipakodi wanapata elimu na mafunzo ya kutosha ili waweze kuutumia mfumo huo kwa ufanisi, jambo litakalosaidia kujenga mahusiano mazuri kati ya mamlaka ya kodi na wafanyabiashara.Kwa upande wao, wafanyabiashara wamepongeza juhudi za Mregi na TRA kwa kutoa mafunzo kuhusu matumizi ya IDRAS, wakisema yameongeza imani na kuondoa migogoro iliyokuwepo hapo awali.Mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam, Pendo Lucas, amesema kwa sasa wafanyabiashara na TRA wanafanya kazi kwa ushirikiano na kujiamini.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment